Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imefanya majlisi ya usomaji wa Qur’ani kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Muharam

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kufuatia kuingia mwezi wa Muharam.

Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani Bibi Manaar Aljaburi amesema “Kikao kimehusisha usomaji wa Qur’ani tukufu, ukafuatia muhadhara elekezi wenye anuani isemayo (Kwa namna gani niwe pamoja na Hussein –a.s-), umetolewa na mwalimu wa Fiqhi katika Maahadi Bibi Zainabu Najaar, amebainisha umuhimu wa niya nzuri, vitendo vyema na kufuata mwenendo wa Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa, kikao kimehitimishwa kwa usomaji wa qaswida na tenzi zilizotaja msiba wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) siku ya Ashura.

Maahadi inaendelea kufanya harakati za kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani, kujenga uelewa wa Dini na kutambulisha historia ya Ahlulbait (a.s) na misingi ya ubinaadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: