Miongoni mwa ratiba ya uombolezaji.. Kitengo cha mahusiano kinaendelea na majlisi za kuomboleza katika ukumbi wa utawala

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala katika siku za mwezi huu wa Muharam.

Majlisi imehudhuriwa na viongozi wengi wa Ataba tukufu, watumishi na zuwaru.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata muhadhara kutoka kwa Shekhe Ali Darii, ametaja sababu zilizompelekea Imamu Hussein (a.s) kufuatana na wanawake na watoto katika msafara wake, nafasi kubwa waliyokuwa nayo katika kufikisha ujumbe kwa umma baada ya mauwaji wa Karbala.

Akafafanua kuwa, Kufuatana na wanawake na watoto ilikuwa ni sehemu ya kutimiza hoja kwa watu na kuonyesha kuwa msafara wa Imamu Hussein (a.s) ulikuwa wa Amani, wenye lengo la kurekebisha umma na kuamrisha mema na kukataza mabaya.

Majlisi hizo ni sehemu ya harakati za kitengo zinazofanywa katika mwezi wa Muharam, kwa lengo la kuomboleza msiba wa Ahlulbait (a.s) na kusambaza elimu na utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: