Kitengo cha mitambo (gari) katika Atabatu Abbasiyya, kimegawa maji kwa mawakibu zilizopo katika mji wa zamani, ikiwa ni sehemu ya huduma za mwezi wa Muharam.
Ugawaji huo wa maji ni sehemu ya kusaidia mawakibu Husseiniyya zinazohudumia zuwaru katika siku hizi za Muharam kulingana na mahitaji yao.
Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake mbalimbali imekuwa ikitekeleza mkakati maalum wa utoaji huduma bora kwa waombolezaji na zuwaru ndani ya mwezi huu mtukufu wa Muharam.



