Njia zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na mji wa zamani hadi katika haram takatifu, kumejaa mawakibu Husseiniyya zilizokuja kuhuisha tukio hilo.
Mawakibu zimetoka maeneo tofauti ya mji wa Karbala, zikiwa zimebeba bendera za uombolezaji na kuimba tenzi zinazotaja namna Abulfadhil Abbasi (a.s) alivyojitolea katika siku ya Ashura.
Kitengo kimeweka mkakati maalum wa kuratibu harakati za mawakibu katika maombolezo ya Ashura, ikiwa ni pamoja na kubaini njia ya kila maukibu na kusimamia matembezi yao ili kuzuwia muingiliano baina ya mawakibu na zuwaru.





