Kitengo cha utumishi kimegawa katoni elfu 25 za maji ya kunywa kwa mawakibu Husseiniyya

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimegawa katoni elfu 25 za maji ya kunywa kwa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vinavyo shiriki katika maombolezo ya mwezi wa Muharam.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Ausi Twahiri amesema: “Ugawaji wa maji umehusisha mawakibu Husseiniyya zilizopo katika eneo linalozunguka haram tukufu, ambapo jumla ya katoni elfu 25 zimetolewa”.

Akaongeza kuwa “Jambo hilo ni sehemu ya huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya kwa mawakibu Husseiniyya ndani ya mwezi wa Muharam, jambo linalosaidia kurahisisha shughuli za uombolezaji kwa zuwaru wanaokuja katika mji mtukufu wa Karbala”.

Kitengo cha utumishi kinafanya kila kiwezalo katika kufanikisha ziara ya Ashura na kutoa huduma bora kwa waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: