Kitengo cha Baina-Haramaini katika Atabatu Abbasiyya, kimegawa maji ya kunywa ya baridi kwa zuwaru wa siku ya mwezi kumi na tatu Muharam kupitia maukibu ya utumishi.
Makamo rais wa kitengo Sayyid Habibu Dahashi amesema: “Kitengo kinatoa huduma mbalimbali kwa zuwaru, ikiwa ni pamoja na ugawaji wa maji ya kunywa muda wote, kupitia maukibu iliyopo katika barabara ya Swahibu Zamani (a.f)”.
Akaongeza kuwa “Kazi hiyo inalenga kupunguza shida kwa zuwaru inayotokana na kuongezeka kwa joto na kuwarahisishia utekelezaji wa ibada ya ziara”.
Kazi hiyo ni sehemu ya mkakati maalum ulioandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unaolenga kutoa huduma bora kwa zuwaru katika siku ya mwezi kumi na tatu Muharam.






