Ofisi ya Sayyid Sistani imejibu swali kuhusu uchafuzi wa mazingira katika taifa la Iraq

Ofisi ya Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu, siku ya Jumatano, imejibu swali kuhusu uchafuzi wa mazingira katika taifa la Iraq, kutiririsha maji yaka, kuenea kwa taka ngumu, kusambaa mabaki ya dawa na kemekali.

Ifuatayo ni nakala ya swali na jibu:

Kwa ofisi ya Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Sistani

Amani iwe juu yenu na rehma yake na Baraka zake…

Hivi karibuni kumekuwa na uchafuzi wa mazingira katika taifa la Iraq, kwa kutiririsha maji taka, kuenea kwa taka ngumu, kusambaa mabaki ya dawa na kemikali za aina mbalimbali zinazoenda kuchafua maji kwa kiwango kikubwa, jambo linaloharibu mazingira na kuhatarisha afya za watu.

Tunaomba ufafanuzi kwa muheshimiwa Marjaa wetu kuhusu swala hili.

Kundi la waumini.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtukufu.

Haifai kutiririsha maji taka, kutupa hovyo taka ngumu, mabaki ya dawa na kemikali, jambo linaloweza kusababisha madhara kwa watu, mwenye kufanya hivyo anapata dhambi na mwenye kusaidia kufanikisha jambo hilo pia, hakuna ruhusa ya kuvunja sheria na maelekezo ya watalam, kwa mamlaka zinazo husika ziweke njia mbadala itakayosaidia kuepukana na tatizo tajwa, aidha ni wajibu kwa kila mtu kufanya mambo kwa hekima na kuwajibika katika mambo yenye maslahi kwa jamii, na Mwenyezi Mungu ndio muongoaji.

Muharam 15/1448h.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: