Wahudumu wa kitengo cha Baina-Haramaini katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kuosha mitambo yao ya kutolea huduma, baada ya kukamilisha kumbukizi ya mazishi ya Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Kazi hiyo imehusisha ukaguzi wa kifundi kwenye mitambo mbalimbali na kufanya ukarabati, ili kuhakikisha mitambo inaendelea kutoa huduma zinazotakiwa.
Ukarabati unalenga kutunza mitambo ili iendelee kufanya huduma kusudiwa na kujiandaa na ibada ya ziara na kuadhimisha matukio ya kidini yajayo.



