Barabara zinazoelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zimeshuhudia mawakibu za waombolezaji zikiwa zimebeba bendera za uombolezaji na kuimba qaswida na tenzi zinazo amsha hisia za majonzi na huzuni.
Kitengo cha maadhimishi kimeandaa mkakati maalum wa kusimamia matembezi ya mawakibu, na kuteua njia maalum za kupita kila maukibu, ili kuepusha msongamano na muingiliano baina ya mawakibu na zuwaru.










