Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu chaita watoto wa mashahidi wa hashdi shaabiy kwa ajili ya kutengeneza ujumbe wa video wawapiganaji.

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetoa wito kwa familia za mashahidi wa hashdi shaabiy (wapiganaji wa kujitolea) zenye watoto wa mashahidi (watoto wa shahidi, ndugu wa shahidi wakiume na wakike) walio chini ya miaka kumi na mbili, kwa wenye kupenda kutengeneza picha za video za wapiganaji, wafike katika shule ya msingi ya Alqamar ya watoto wa kike, iliyopo katika mtaa wa Hussein (a.s), mkabala na (swiming pool) ya Karbala ya Al aulambi kuanzia siku ya Juma Mosi (31 Desemba 2016 m) na kila siku za Juma Mosi zitakazo fata.

Ifahamike kua: video hizo zitawekwa katika toghuti maalumu ya fatwa ya kujilinda na zitaonyeshwa rasmi katika kongamano la fatwa ya kujilinda litakalo endeshwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu la kila mwaka kwa mnasaba wa kutolewa kwa fatwa ya kihistoria, iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji mtukufu wa Najafu, ambayo ilipokelewa vizuri na raia wa Iraq na wakajitokeza kulinda aridhi, heshima na maeneo matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: