Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chakamilisha maandalizi ya awamu ya pili ya kukomboa magharibi ya mji wa Mosul na mkuu wao asisitiza umuhimu wa kukombolewa kwa vitongoji vyote vya Tal’afar..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilika kwa maandalizi ya awamu ya pili ya vita vya kukomboa magharibi ya Mosul chini ya kauli mbiu ya (Tunakuja ewe Nainawa) makomando wa kikosi wapo katika maandalizi kamili ya kukomboa sehemu zilizo bakia katika umiliki wa daishi na wameahidi kuwapa somo ambalo hawatalisahau kamwe.

Naye kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidi alisisitiza kua: “Hakika viongozi wa juu wanaona jambo la kwanza litakua ni kukomboa vijiji vyote vilivyopo pembezoni mwa Tal’afar chini ya kauli mbiu (Tunakuja ewe Nainawa) kwa sababu awamu ijayo ni awamu ya kushinda vita, ili kushinda vita ni lazima tukomboe maeneo yote ya Tal’afar, kwa sababu kukombolewa kwa Tal’afar yote ni sawa na kukombolewa kwa Mosul”.

Ikumbukwe kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilikua na ushiriki mkubwa katika awamu ya kwanza ya kukomboa magharibi ya Mosul, na kilifanikiwa kukomboa takriban kilometa (300) pamoja na makumi ya miji na vijiji, pia kilitoa misaada ya kibinadamu na kuwazirudisha familia nyingi za wakimbizi katika maeneo ya makazi salama, kikosi cha Nukhba, na uingiliaji wa haraka vinaendelea kulinda maeneo ya kimkakati na wapo katika maandalizi kamili ya kushambulia wakati wowote itakapo hitajika.

Vikosi vitakavyo shiriki ni: kikosi cha vifaru, kikosi cha mizinga, kikosi cha Ummul Banina (a.s), kikosi cha Alwiyatul Kafeel, kikosi cha Alqamiy pamoja na kikosi cha anga (ndege), na kikosi cha uangalizi wa kimtandao na kikosi cha wapelelezi, na watashiriki wapiganaji wengine kutoka katika kikosi cha imam Ali (a.s) kilicho chini ya Atabatu Alawiyya tukufu, na Liwaau Answaaru Marji’iyya, na wapiganaji wa Muhammad Asgharu walio chini ya Mazaru ya Sayyid Bakari bun imam Ali (a.s) katika mji wa Babil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: