Atabatu Abbasiyya tukufu yakirimu familia za mashahidi na yasisitiza kua inacho kitoa hakifikii tone moja la damu ya shadidi iliyo dondoka kwa ajili ya kuihami Iraq na maeneo yake matukufu..

Sehemu ya hafla ya kuwakirimu
Atabatu Abbasiyya tukufu imesisitiza kua, hakika wanacho kitoa hakifikii hato uzito wa tone moja la damu iliyo dondoka kwa ajili ya kuhami Iraq na maeneo yake matukufu, na hakika wanacho kitoa kwa familia za mashahidi ni kidogo sana ukilinganisha na jinsi wao walivyo jitolea kwa ajili ya kunusuru dini na madhehebu pamoja na kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu, hakika wamekua ngoa imara ya kuzuia magaidi ya kitakfiri, wao ndio fahari ya Iraq na utukufu wake.., haya yalizungumzwa na kiongozi wa msafara wa Ataba tukufu Shekh Maajid Sultani wakati akikabidhi zawadi kwa familia za mashahidi katika mkoa wa Baabil kitongoji cha Shomaliy.

Alisema kua: “Hakika zawadi hizi, zinatokana na msimamo wa kibinadamu walio nao Atabatu Abbasiyya tukufu, naimani yao ya kuendelea kuwasiliana na jamii za wairaq, hasa familia za watu walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu na wakajitolea damu zao kwa ajili ya kuhami nchi na maeneo matukufu. Hii ni sehemu ya ratiba ya kitengo cha dini katika atabatu Abbasiyya tukufu ya kuwatembelea na kuwapa zawadi familia za mashahidi bila kujali dini na mielekeo yao, wanaendelea na kazi hii iliyo anza katika siku za mwanzo za kutolewa kwa fatwa tukufu ya jihadi difaai (kujilinda)”.

Sultani akafafanua kua: “Ziara hii ya kuwakirimu familia za mashahidi imefanyika katika mkoa wa Baabil kitongoji cha Shomaliy imehusisha familia (14) za mashahidi katika kikao kilicho fanyika ndani moja ya misikiti ya eneo hili kwa kusaidiana na taasisi ya Imam Mujtama (a.s)”.

Akaendelea kusema kua: “Kitongoji cha Shomaliy kina idadi kubwa ya mashahidi wanazidi mia moja, na wengi wao walikua katika jeshi la umoja, kwa hiyo tutakua na ziara zingine katika kitongoji hiki kwa ajili ya kuendelea kuwakirimu familia zingine, tumewaambia familia za mashahidi kua, zawadi hizi zinatoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tena katika masanduku ya Hashdi sha’abiy yaliyopo katika haram hiyo, hakika zawadi hizi si lolote ukilinganisha na jinsi walivyo jitolea watoto wao, na tuliwaambia pia zawadi hizo wazigawe kwa watu wa familia”.

Familia za mashahidi walishukuru sana kwa zawadi hizo na wakasema, hakika zawadi hizi zinatujenga kimaanawiya zaidi na zinatushajihisha kuendelea na mapambano hadi tuwamalize magaidi ya kidaesh na tuitwaharishe aridhi ya Iraq kutokana na uchafu wao.

Kumbuka kua; Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu ya kuzisaidia familia za mashahidi na majeruhi, imeandaa ratiba kamili ya kutembelea mfulilizo familia za mashahidi na majeruhi katika mikoa yote ya Iraq bila kutofautisha, kwa ajili ya kua karibu nao na kuwasaidia, misaada inayo endana na kujitolea kwa watoto wao, ziara hizi zinaendelea mfululizo hadi tuwafikie familia zote za mashahidi walio pata shahada kuanzia tarehe iliyo tolewa fatwa ya wajibu kifai (jihadi ya kujilinda).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: