Hivi punde.. kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chasonga mbele katika kukomboa kijiji cha Darnaji..

Maoni katika picha
Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetangaza kusonga mbele kwa wapiganaji wake pamoja na kikosi cha 36 cha jeshi la serikali katika kukomboa kijiji cha Darnaji kilichopo upande wa kulia wa mji wa Mosul chini ya kauli mbiu ya (Tunakuja ewe Nainawa) wamefanikiwa kuwapa hasara kubwa magaidi ya daesh ikiwa ni pamoja na kuwaua magaidi (15) wengi wao sio raia wa Iraq, bado mapambano yanaendelea hadi kukombolewa kwa kijiji chote ambacho kijeshi ni sawa na kimesha kombolewa, kipo chini ya mashambulizi makali ya jeshi.

Kwa upande mwingine wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamefanikiwa kuwakamata magaidi tisa (9) waliokua wamejificha ndani ya nyumba katika eneo la Tilal-atshana upande wa kulia wa mji wa Mosul.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: