Kuanzishwa kwa mtandao wa kituo cha Ameed Duwaliy lilbuhuthi wa dirasaat..

Maoni katika picha
Kituo cha Ameed duwaliy lilbuhuthi wa dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanzishwa kwa mtandao wake maalumu utakao rusha harakati zake, mtandao huo utakua moja ya njia muhimu za mawasiliano.

Sekertali mkuu wa kituo hicho Ustadh Ridhwan Abdulhaadi Salami amesema kua: “Mtandao huu umesanifiwa na kupangwa program zake na wataalamu wa kituo cha uzalishaji cha Maahadi Alkafeel chini ya idara ya Intanet, na unasehemu zifuatazo: Sehemu za kituo, Habari, Machapisho, Wajumbe wa kituo, Makongamano, Ripoti za semina na taarifa kuhusu harakati, pia kuna jarida la Ameed ambalo linaandika maswala ya kitafiti na masomo ya kibinadamu, jarida la Baahir Al-ilmiyya linalo andika maswala ya mazingira na kihandisi na jarida la Taslim linalo andika fani za lugha ya kiarabu.

Akaongeza kusema kua: “Hakika mtandao huu umesanifiwa kisasa zaidi na kupangiliwa vizuri mno, hakika hatua hii ilitarajiwa na tunaendelea kufanya juhudi hadi ifikie hatua ya kurusha matangazo ya kituo cha Ameed duwaliy lilbuhuthi wa dirasaat kupitia mtandao mkuu.

Unaweza kutembelea mtandao huu kupitia anuani ifuatayo:

http://alameedcenter.iq/index.pho
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: