Zaidi ya vitabu elfu 16: Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao yazindua App ya kiitikadi..

Maoni katika picha
Miongoni mwa App zake katika simu za kisasa (smartphone), Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imezingua App ya mtandao wa marejeo ya kiitikadi katika simu za kisasa (smartphone) katika (ios) kama hatua ya kwanza na kisha kuingia katika (Android) App hii inazaidi ya vitabu elfu 16 vinavyo jibu shubha (utata) mbalimbali kwa dalili za pande mbili, “upande wa Ahlulbait (a.s) na upande wa Ahlusunna” na kuna milango mingi, miongoni mwa milango hiyo ni: Riwaya, Dhulma alizo fanyiwa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), pamoja na mada zenye uhusiano wa kiitikadi zinazo jibu utata (shubha). App hii imeingizwa katika dirisha la Mtumishi wa Ahlulbait (a.s) kutokana na ruhusa ya kisheria iliyopo katika App hiyo.

Unaweza kupakua App hii kwa moja ya njia mbili za Android:

https://play.google.com/store/apps/details? id=turath.alanbiaa.app.almarjea_alakaede

Kumbuka kua Maahadi ya turathi za mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao ni moja ya asazi zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa malengo yake ni:

  1. Kujenga jamii inayo mtambua Mungu na yenye maadili mema.
  2. Kushajihisha wanafunzi na watafiti, waongeze juhudi katika masomo au tafiti zao kwa kuwarahisishia upatikanaji wa mambo wanayo hitaji katika fani zao wanazo somea au kutafiti.
  3. Kusambaza elimu ya Ahlulbait watakasifu (a.s) kwa anaehitaji katika kila kona ya Dunia. Hususan masomo ya hauza (Dini) kwa njia ya mtandao nyepesi na rahisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: