Inatokea sasa hivi: Mamilioni ya watu wanaendelea kumuomboleza Imamu Hussein (a.s) katika siku ya tisa..

Maoni katika picha
Unanitisha kwa mauti.. kuuawa mara elfu kwa panga pamoja na Hussein ni pora kwangu kuliko kuishi pamoja na nyie..

Maneno haya aliyasema, Shahidi Sayyid Zuhairu bun Qain, kumuambia mmoja wa waovu wa jeshi la ukafiri la Umawiyya alipo karibia kuuawa.

Msimamo huu imara na uaminifu mkubwa ulionekana katika makundi makubwa ya waombolezaji na mazuwaru walio itikia agizo la Mola mtukufu la kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume (a.s), waliotoka na kuelekea Karbala kwenda kumzuru bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s), katika kumbukumbu ya kuuawa kwake na kufanya maombolezo katika kaburi lake takatifu, huku wakitangaza kushikamana na msimamo wake mtukufu.

Uhalisia wa mazingira yao unasema:

Pamoja kua hatukusimama na wewe katika viwanja vya Twafu..

Hakika tumekuitikia japo baada ya zama nyingi.. kwa kusema Labaika yaa Hussein, maini yetu yamechemka kwa hasira, na nyoyo zimejaa mapenzi, misafara na misafara inakuja kuomboleza na kufanya taazia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: