Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaudhibiti mji wa Riyaadh na chaanza kazi ya kuusafisha.

Maoni katika picha
Kutokana na ushirikiano wa jeshi la anga, kikosi cha Abbasi (a.s) brugedi ya 26, kimefanikiwa kuukomboa mji wa Riyaadh uliopo kusini ya mji wa Huweja kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh, katika opresheni ya (Tunakuja ewe Huweja) awamu ya pili ya opresheni hiyo, na wameanza kazi ya kuusafisha mji huo kwa kutegua mabomu na vilipuzi vilivyo tegwa na magaidi ya Daesh.

Kwa upande mwingine, kikosi hicho kwa kusaidiana na brugedi ya 16 ya (Hashdi Turkumani), wamefanikiwa kukomboa vijiji vya (Saami-Aaswi, Saadah, Talah-Jul, Hamirah-Swaghirah, Hamirah-Kabirah, Yarghunul-Ulya, Yarghunu-Sufla na Majbal).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: