Kimbunga cha kumpenda Hussein ni kikubwa kushinda vimbunga vya vumbi na kubadilika kwa hali ya hewa..

Maoni katika picha
Hawajali wala hawaangalii kubadilika kwa hali ya hewa na wingi wa vimbunga vya udongo wala ugumu wa njia na umbali wa masafa..

Hawa hapa wapenzi wa watu wa nyumba ya Mtume wanachapa mwendo..

Wakitumia njia kubwa na ndogo..

Wakikusudia kumzuru Abu Abdillahi Hussein (a.s)..

Wanapita kila njia wanayo amini itawafikisha Karbala..

Huku hali ya mazingira yao ikisema: Iwapo maadui wa Hussein wakikata mwili, mapenzi ya Mola yatambakiza Hussein katika roho ya kila anaye sema (Laa ilaaha ila Llah.. Muhammad Rasulu Llah).

Hizi ni sehemu za picha za mazuwaru wanaotembea kwa miguu katika mji wa Batwihaau uliopo katika mkoa wa Dhiqaar, na katika wilaya ya Hadhar mkoa wa Muthanah.

Kumbuka kua mikoa mingine ya kusini kama vile Misaan, Diwaaniyya na Baabil hadi Karbala, imeshuhudia makundi makubwa ya watu wanaoenda kufanya ziara, tutakuleteeni habari kamili baada ya kurejea waandishi wetu waliopo huko.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: