Hivi punde… baada ya miaka mitatu ya vita kikosi cha Abbasi (a.s) chapumzisha siraha zake…

Maoni katika picha
Katika muonekano wa aina yake na unyenyekevu mkubwa, majemedari wa Alkafeel miongoni mwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wapumzisha siraha zao, deraya, vifaru na mabomu, vifaa vilivyo wapa hasara kubwa magaidi wa Daesh katika kila vita waliyo pigana, na hawakushindwa vita yeyote dhidi ya magaidi hao.

Sababu za kupumzisha siraha zao ni kutokana na maelekezo kutoka kwa viongozi wao, baada ya kuwasili kwa wapiganaji hao katika eneo la mpaka wa Iraq na Sirya, na kujikuta wako mbele ya aridhi ya bibi mtukufu wa Sham bibi Zainabu (a.s), kutokana na ishara ya haiba na unyenyekevu wa bibi huyu mtakasifu aliye lelewa katika nyumba ya utume bint wa Zaharaa (a.s).

Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi wamefuta machozi katika mpaka huu, na kutuma salamu kwa bibi mtukufu wa Sham, kisha wamerejea kutekeleza malengo yao wakisema (Labaika yaa Iraq), na wametangaza kupata ushindi wa mwisho dhidi ya magaidi wa Daesh katika ngome yao ya mwisho ya mji wa Qaaimu, wakitangaza kua risasi ya rehema imekua mwiba mkali kwa magaidi hao, sasa nchi itasherehekea ushindi wa mwisha, na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwanusuru waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: