Kuanza kwa program ya ujumbe kwa watoto katika njia ya Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Kufuatia ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na kama sehemu ya harakati zake katika ziara hii, Maahadi ya turathi za mitume na masomo ya hauza kwa jia ya mtandao, chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameanzisha program ya (Ujumbe kwa watoto) inao walenga watoto wano kwenda ziara kwa Imamu Hussein (a.s).

Program hii iliyo anzishwa katika mgahawa (mudhifu) wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kufundisha maadili mema kwa watoto yanayo tokana na mafundisho ya kifiqhi na kiaqida, pamoja na kuwajengea uzalendo unao endana na akili zao na umri wao, yameandaliwa maswali mengi na watu walio bobea katika elimu za watoto, yanayo ulizwa kwa njia ya mazungumzo na kwa namna inayo vutia na kukubalika kwa watoto, maswali hayo yanamuwezesha kila mtoto kusema kilicho moyoni mwake na kueleza kinacho msukuma kufanya matembezi haya, na kiwango cha uwelewa wake kuhusu Imamu Hussein (a.s) na muhanga wake mtukufu, pia anaelezea usalama wa watoto, pamoja na maswali yanayo husu uwelewa wake wa dini na mengineyo.

Mazungumzo hayo yanapigwa picha za mnato na za video na kila mtoto anapewa zawadi, ambayo ni mkufu wenye kisidii (cd) cha dhahabu chenye nakshi ya maandishi yasemayo (Yaa Abalfadhil Abbasi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: