Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji chasema: Tutafunga mpaka katika hatua ya mwisho ya vita…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Shekh Maitham Zaidiy asubuhi ya leo Alkhamisi (18 Rabiul-Awwal 1439h) sawa na (7 Desemba 2017m) ametangaza kua wapiganaji wake wamejikusanya katika mpaka wa Iraq na Sirya, wakiwa tayali kuanza hatua ya mwisho ya vita inayoitwa (Vita ya kisiwa kikubwa).

Akasema kua; jukumu walilo pewa ni kukomboa eneo la mpakani linalo unganisha Iraq na Sirya na kufunga mpaka baada ya kumaliza kuua Daesh wa mwisho katika ardhi ya Iraq, kisha kutangaza kua mpaka wa Iraq ni mstari mwekungu kwa gaidi yeyote, hataruhusiwa kuvuka mpaka huo, Shekh Zaidiy ameonyesha imani kubwa kwa wapiganaji wake kua na uwezo wa kushinda vita kwa muta tarajiwa kama walivyo shinda vita zingene, pamoja na ukubwa wa eneo hilo.

Katika vita hii vitashiriki vikosi vyote, kikosi cha deraya, mizinga, mabomu pamoja na wapiganaji kutoka katika vikosi vingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: