Nje ya ofisi na mbele ya makumi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Sayyid Swafi anatoa darsa la akhlaq kila siku kwa kusherehesha dua ya Abu Hamza Shimali…

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani, ni mihadhara inayo tolewa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kila siku jioni, katika sardabu ya Imamu Kadhim (a.s) iliyopo ndani ya Ataba tukufu, anasherehesha dua na munajaat Abu Hamza Shimali, ambayo ni miongoni mwa dua za usiku zilizo pokewa na Imamu Zainul-Aabidina (a.s), mihadhara hiyo huitoa kwa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikiwa kama sehemu ya kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mihadhara na sherehe za vipande vya dua vilivyo jaa mafundisho ya akhlaq na malezi katika dua hiyo mashuhuri kutoka kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s) hususan katika mwezi wa Ramadhani.

Kituo cha uzalishaji na upigaji picha cha Alkafeel kila siku kinarekodi mihadhara hiyo na kuirusha katika masafa maalumu inayo tumika kurushia matangazo ya mwezi wa Ramadhani kuanzia saa sita (6:00) usiku.

Unaweza kufuatilia matangazo hayo kupitia anuani zifuatazo:

SAT:INTELSAT 902@62°E:
DL:11457.5V
SR:3000
DVBS2
8PSK
FEC 2/3
HD/MPEG-4
pia unaweza kupata matangazo mubashara kupitia youtube:

https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw
na kupitia facebook:
https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: