Kikosi cha Atabatu Abbasiyya cha wapiganaji chaaga msafara wa kwanza wa mahujahi na mkuu wa kamisheni ya Furaat Ausat apongeza juhudi zao za kuimarisha usalama katika mkoa wa Karbala…

Maoni katika picha
Baada ya kuanza kutekeleza jukumu la ulinzi wa amani katika barabara ya (Nakhibu – Ar’ur), wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wameiaga misafara ya watu wanaokwenda hija kupitia barabara, wameishindikiza misafara hiyo hadi umbali wa zaidi ya kilometa (80) kuanzia mji wa Faaji hadi Nakhibu, sambamba na kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo kufuatia uwepo wao endelevu, mahujaji hao wametokea katika mikoa ya Muthana, Misaan na Karkuuk.

Kwa upande mwingine kamanda wa kamisheni ya Furaat Ausat Qais Khalf Rahima Almahmadawi amesifu kazi nzuri inayo fanywa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) ya kuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa mtukufu wa Karbala, kuanzia vitisho vya mara ya kwanza vilivyo pewa mkoa huo hadi sasa, na kuimarisha ulinzi katika misafara ya mahujaji ni dalili ya wazi kuhusu utekelezaji mzuri wa majukumu yao, hilo ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi yao ya kuimarisha ulinzi na usalama katika miji waliyopo.

Kumbuka kua kikosi hiki kilikua kimesha tangaza kuimarisha ulinzi katika barabara inayo elekea Saudia (Nakhibu – Ar’ur) kupitia bulged tatu kikiwemo kikosi cha deraya, baada ya kupewa rasmi jukumu hilo na kamisheni ya Furaat Ausat katika kikao kilicho fanywa mwezi huu kwenye makao makuu ya kikosi.

Ni vizuri kukumbusha kua sehemu ya wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wanalinda amani katika mji wa Nakhibu tangu miaka mitatu iliyo pita chini ya uangalizi wa kamisheni ya Furaat Ausat na haujawahi kutokea uvunjifu wa amani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: