Ukurasa wa picha za videa ni njia ya kuona harakati mbalimbali zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma mbalimbali za kiutumishi na kiujenzi, pamoja na mambo ya kielimu na kitamaduni, mtandao wa kimataifa Alkafeel ukizingatia kua ndio chombo cha habari kikuu na mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, umeandaa ukurasa maalumu wa picha za video, unao onyesha video za kila kinacho fanywa na Atabatu Abbasiyya, ukurasa huo unaitwa (maktaba ya picha za video) unapatikana kupitia anuani ifuatayo: (https://alkafeel.net/videos) katika ukurasa huo huonyeshwa picha za video zilizo pigwa kwa ustadi mkubwa, ili kumuwezesha mtazamaji kufahamu harakati mbalimbali zinazo fanywa na Ataba katika sekta ya utamaduni, utumishi, ujenzi na nyinginezo, huwekwa picha za video za mambo mapya yanayo fanyika.

Ofisi ya picha za video inajumuisha picha za makongamano, mikutano, nadwa zinazo fanywa au kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na mihadhara ya dini inayo tolewa ndani ya uwanja wa haramu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na mahafali za Qur’ani na visomo vya mashairi na kaswida vinavyo fanyika ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na khutuba za Ijumaa zinazo swaliwa katika uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s), pia kuna picha za habari na baadhi ya mafanikio muhimu yaliyo fikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo na vituo vyake pamoja na taasisi zake.

Ukurasa huo pia unaripoti za picha za miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta zote, ili kumuwezesha mtazamaji kuielewa kwa urahisi, mambo hayo yanafanya ukurasa huu kua hazina ya mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: