Kikosi cha kuigiza Aljuud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimepata tuzo tatu mwoshoni mwa kongamano la Hussein mdogo kwa maigizo ya watoto.

Maoni katika picha
Kikosi cha kuigiza Aljuud chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kimepata tuzo tatu katika kongamano la kimataifa awamu ya tano kuhusu uigizaji wa watoto Husseini mdogo awamu ya tano, yaliyo simamiwa na kitengo cha malezi na makuzi ya mtoto katika Atabatu Husseiniyya tukufu.

Tuzo zimepatikana kutokana na igizo lililokua na anuani isemayo (usiseme kaukau), igizo hilo limepata tuzo ya igizo bora, iliyo kwenda kwa Zainabu Azawi, na tuzo ya maandishi bora, pamoja na tuzo ya kaswida bora iliyo kwenda kwa Jaliil Khuz-ali.

Vilevile (igizo hilo) likapendekezwa kupata tuzo tatu zingine ambazo ni tuzo ya kazi bora iliyo kamilika, tuzo ya senografu bora na tuzo ya kamati tendaji.

Fahamu kua kongamano la Hussein mdogo linalo husu maigizo ya watoto ni miongoni mwa makongamano muhimu hapa nchini, linaujumbe wa aina mbalimbali kwa watoto, ikiwa ni pamoja na kujenga uzalendo wa taifa lao sambamba na hisia za kupenda kufanya mambo mazuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: