Kumliwaza wanaemtumikia: Watumishi wa Alkafeel wanatoa pole katika kumbukumbu ya kifo cha dada yake jabali wa subira.

Maoni katika picha
Kufuatia kauli ya bibi Zainabu (a.s) alipo simama kama nguzo mbele ya Yazidi na vibaraka wake, akazungumza kwa kujiamini na ushujaa: (…Fanya vitimbi vyako na ongeza juhudi yako, wallahi hautafuta utajo wetu wala hauta uwa mafundisho yetu), katika uombolezaji wa watumishi wake na wahudumu wa mazuwari wake, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya Adhuhuri ya Jumamosi (15 Rajabu 1440h) sawa na (23 Machi 2019m) wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha bibi Zainabu.

Matembezi yalianzia katika malalo ya mtumishi wa Hauraa na mbeba bendera mkarimu Abulfadhil Abbasi (a.s), wametoa pole zao kupitia kaswida na mashairi mbele ya malamo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha wakaelekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kufanya majlisi ya kuomboleza, wakasoma kaswida na mashairi yaliyo elezea dhulma alizo fanyiwa Hauraa Zainabu (a.s).

Katika maukibu hiyo wameshiriki viongozi wengi na watumishi wa Atabatu Abbasiyya, wakiongozwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi (d.t) pamoja na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati kuu, na kundi la mazuwaru waliokuja katika mji wa Karbala kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: