Baada ya mwaka na nusu tangu wapate ushindi wa kihistoria: Askari wa kujitolea wa Hashdi Shaábi wanasoma Quráni ndani ya harama ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Kama zilivyo lia bunduki za wapiganaji wa Hashdi Shaábi katika uwanja wa vita na kuwashinda maadui wa Iraq Daesh na wengine, leo baada ya mwaka na nusu wa ushindi wa kihistoria uliolinda ardhi na heshima pamoja na kuhami maeneo matukufu, wanapaza sauti zao kwa kusoma aya za Quráni tukufu ndani ya Atabatu Abbasiyya, kupitia kitengo cha Quráni cha Hashdi Shaábi, katika mradi wa (Arshu Tilawa) wa kila wiki.

Hafla ilishuhudia usomaji tofauti kutoka kwa washiriki, ilifunguliwa kwa kisomo kilicho burudisha wahudhuriaji, cha msomaji wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa Mauhubu Swadiq Fariji, kisha akasoma bwana Ahmadi Khalfu, halafu akasom bwana Muhammad Abdu Shahidi, na wakahitimisha kwa usomaji wa pamoja wa kikosi cha mashahidi wa Hashdi Shaábi waliogusa nyoyo za waumini.

Kumbuka kua hafla imepata mahudhurio makubwa pamoja na waandishi wa habari kutoka katika chanel ya Quráni tukufu ambayo ipo chini ya chanel za Karbala na kituo cha uzalishaji cha Alkafeel ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: