Maoni katika picha
Makamo kiongozi wa kituo cha uzajishaji na matangazo mubashara Alkafeel Ustadh Iswaam Mussawi amesema kua: “Lengo la kuanzishwa kituo hiki ni kufikisha ujumbe wa Atabatu Abbasiyya na miradi yake kwa walimwengu”.
Akaongeza kua: “Miongoni mwa malengo muhimu ya kuanzishwa kwa kituo hiki ni kupunguza msongamano ambao hutokea katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kwa kupunguza idadi ya gari za matangazo ya mubashara pamoja na vyombo vya habari, sisi huandaa masafa ya kurusha matangazo mubashara bure kwa vyombo vyote vya habari vinavyo taka kurusha matukio ya ziara”.
Fahamu kua kituo cha uzalishaji na matangazo mubashara Alkafeel kutokana na kazi nzuri kinayo fanya kimekua miongoni mwa vituo bora vya utangazaji.