Ilitokea siku kama ya leo mwezi kumi na tisa Muharam 61h: Kuondoka mateka wa Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Kufa kwenda Sham

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi kumi na tisa Muharam mwaka wa 61h, msafara wa mateka uliondoka katika mji wa Kufa kwenda Sham wakitanguliwa na vichwa vya mashahidi, vikiongozwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s), baada ya Yazidi kumuandikia barua Gavana wake wa Kufa Ubaidullahi bun Ziyadi ya kumtaka awapeleke mateka kwake, katika barua hiyo alisema: (Walete kwangu mateka) kwani alitaka kufurahisha nafsi yake kwa kuangalia familia ya Mtume (s.a.w.w) inasimama mbele yake ikiwa imefungwa minyororo, Ibun Ziyadi akamwita Makhfar bun Tha’alaba Aaidhiy, akampa vichwa vya mashahidi pamoja na mateka wanafamilia ya Mtume (a.s), akamuambia yeye pamoja na Shimri bun Dhijaushen wawapeleke kwa Yazidi huko Sham.

Msafara wa mateka uliondoka Kufa kwenda Sham ukitanguliwa na vichwa vya mashahidi ambao miili yao ilibaki katika jangwa la Twafu, vikitanguliwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s), nyuma ya vichwa hivyo wakapangwa wanawake na watoto, wakitanguliwa na bibi Zainabu (a.s) jemedari wa Karbala, aliye endeleza harakati ya Imamu Hussein (a.s) kwa njia ya maneno na sio upanga, akiwa na mtoto wa kaka yake Imamu Zainul-Abidina (a.s) aliyekua amefungwa minyororo mikono yake na kuwekwa shingoni kwake, walipanda ngamia zisizokua na tandiko katika msafara wao wa kwenda Damaska.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: