Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s): Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda Atabatu Abbasiyya tukufu, kuta na korido zake zimewekwa mapambo meusi, kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) kilicho tokea siku kama ya kesho mwezi nane Rabiul-Awwal, zimepandishwa bendera za msiba na yamewekwa mabango yenye ujumbe wa kuomboleza ndani ya haram tukufu, kama sehemu ya kuomboleza msiba huu unao umiza roho ya kila muumini na mfuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kila tukio linalo husu kumbukumbu ya kifo cha Ahlulbait (a.s), imeandaa ratiba ya kuomboleza yenye vipengele vingi, kuna utowaji wa mihadhara ya Dini na kufanya majlisi za kuomboleza pamoja na matembezi ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kama sehemu ya kuomboleza msiba huo adhim.

Kumbuka kua wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani wanaomboleza msiba huu na kumpa pole Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) kufuatia kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), aliye uliwa na mtu muovu zaidi, alipewa sumu kali na Mu’tamadi Abbasi iliyo muuguza kwa siku kadhaa adi kifo chake, akiwa na miaka ishirini na nane, alikufa mwezi nane Rabiul-Awwal mwaka wa (260h).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: