Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kusaidia wapiganaji wa Hashdi Shaábi.

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea mji wa Mosul katika wilaya ya Hadhar, kwenda kusaidia wapiganaji waliopo huko, ziara hii ni muendelezo wa ratiba maalum ya kusaidia wanajeshi na Hashdi Shaábi, ambao wamekua wakipambana bila kuchoka tangu ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda hadi leo.

Tumeongea na Shekh Aadil Swalehe Muhammad ambaye ni muwakilishi wa makamo rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amesema kua: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tumeandaa ujumbe huu na kuja kutembelea ndugu zetu wapiganaji wa Liwaa 44 (Answaar Marjaiyya) katika mji wa Hadhar, tumekuja kuwapa moyo na kuwasaidia”, Akasema: “Kwa kweli tulipo watembelea tumewakuta wakiwa na msimamo madhubuti wa kuendelea kupambana na adui, wapiganaji hawa watukufu hawachoki wala hawarudi nyuma katika kupambana na adui wa Dini na taifa”.

Akaongeza kua: “Katika msafara huu tumewapa baadhi ya vitu wanavyo hitaji miongoni mwa vyakula na vitu vingine”.

Sayyid Hamiid Yaasir kamanda wa Liwaa Answaar Marjaiyya amesema kua: “Tumepokea ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo mara nyingi imekua ikituletea marashi kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) na baraka zake, Ataba hii imesimama pamoja na sisi tangu siku ya kwanza ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda, kuanzia miji ya kusini mwa Bagdad, Faluja hadi Swalahu-Dini na kwenye mpaka wa Iraq na Sirya pamoja na hapa katika wilaya ya Hadhar, tunapo fikiwa na ugeni huu mtukufu hutupa nguvu na moyo wa kuendelea kupambana katika jihadi hii takatifu”.

Akasisitiza kua: “Tumeshikamana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, ambaye amekua daima anawasiliana nasi na kutupa moyo, leo tupo katika wilaya ya Hadhar tunaendelea kufanyia kazi fatwa yake tukufu, tumesimama imara kupambana na magaidi wa Daesh na kusafisha mabaki yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: