Ushiriki wa aina yake wa Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano la Twafu la kimataifa awamu ya tisa…

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa ushiriki wake katika maonyesho na makongamano ya kitaifa na kimataifa, Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika kongamano la Twafu awamu ya tisa linalo simamiwa na uongozi wa wakfu shia kwa kusaidiana na chuo kikuu cha Mustanswiriyya kitivo cha adabu chini ya kauli mbiu isemayo (Muhanga wa Imamu Hussein ni mradi wa haki za binadamu).

Kwa mujibu wa maelezo ya Shekh Mahmudu Swafi kutoka katika Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, “Kongamano hili lilihusu kuonyesha vifaa kale vilivyopo katika kituo kama mfano na kuonyesha namna ya kuvikarabati na kuvitunza, pamoja na zana zinazo tumika katika shughuli hiyo, hali kadhalika kuonyesha vitabu vya zamani vya asili na kopi pamoja na kubainisha njia iliyo tumika kuvikopi”.

Kumbuka kua kongamano la Twafu la kimataifa awamu ya tisa, linalo simamiwa na uongozi wa wakfu shia kwa kusaidiana na chuo kikuu cha Mustanswiriyya litakua la siku mbili, na linafanyika ndani ya kumbi za chuo hicho, limepata ushiriki mkubwa wa watafiti wa kiiraq na kiarabu wakiwemo wanaotoka katika nchi za kiajemi, na wamejikita katika tafiti za muhanga wa Imamu Hussein (a.s) na nafasi yake katika islahi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: