Katika mji wa Najafu siku baada ya siku maendeleo yanaonekana wazi katika ufungaji wa mbao za zirisha na mapambo yake, uzuri wa dirisha hilo umeanza kuonekana bayana.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi matukufu na milango ya kwenye malalo takatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao ndio walio liunda na kulifunga dirisha hilo, Sayyid Naadhim Gharabi amesema: “Hakika kazi ya kufunga vipande vya dirisha la Swafi-Swafa inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa”.
Akaongeza kua: “Miongoni mwa kazi zilizokamilika ni kuweka maandishi ya Quráni yanayo fuatiwa na ufito wa dhahabu, maandishi hayo yametengenezwa kwa madini ya silva, imeandikwa surat Nnabaa inayo anza na (Kitu gani wanacho ulizana* Ni kuhusu habari kubwa) na kuishia na (Laiti ningekua udongo) imeandikwa kwa na mwalimu wa hati Dokta Raudhwani Bahiyya kwa hati ya Thuluth murakkab”.
Amebainisha kua: “Kimo cha maandishi ni (sm19) na urefu wake ni (sm4.93 x sm3.82) na unene ni (mlimita7) yamezunguka dirisha pande zote, yamekatwa kihandisi kwa kuzingatia kila kipande na sura yake kwa namna ambayo haviathiri asili ya sura na haraka zake, herufi zimetiwa dhahabu halisi na mina ya bluu”.
Akasema kua: “Maandishi hayo yamewekwa kwa umaridadi mkubwa, nayo ni katika vitu vya ziada vilivyo wekwa na watekelezaji wa mradi huo, wametumia njia za kisasa zaidi katika uwekaji wa maandishi, yanakua yanaonekana pamoja na sehemu zingine kama vile kitu kimoja”.