Jioni ya jana Jumanne (7 Rajabu 1441h) sawa na (3 Machi 2020m), Atabatu Zainabiyya tukufu imefanya hafla ya kuzindua taji la dirisha la kaburi la bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya, lililotolewa na Atabatu Abbasiyya na kutengenezwa katika kiwanda chake cha kutengeneza madirisha na milango ya malalo takatifu.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni maalum kutoka Atabatu Abbasiyya wakiongozwa na mkuu wa ofisi ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Adnani Mussawi, na katibu mkuu wa Atabatu Zainabiyya pamoja na watumishi wa malalo hiyo takatifu na kundi kubwa la waumini, wakiwemo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, iliyo fuatiwa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Adnani Mussawi, akasema kua:
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Muhammad Al-Jawaad (a.s), enyi wahudhuriaji watukufu, kwanza amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu, pili juu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na salam na maamkizi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na Mheshimiwa katibu mkuu na kamati kuu ya uongozi, sambamba na salam na maamkizi ya wageni waliokuja katika Maqaam ya bibi Zainabu (a.s) kumtumikia kwa kufunga taji juu ya kaburi lake takatifu.
Akaongeza kua: “Kama mnavyo tambua Atabatu Abbasiyya hutekeleza miradi yake kwa umakini na ustadi mkubwa, kwa namna ambayo hupendeza katika macho ya watazamaji na mazuwaru, miradi yake inamwanzo wenye nuru na haina mwisho kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nayo ni miradi ya kielimu, kitamaduni na kibinaadamu”.
Akafafanua kua: “Bila kusahau miradi ya ujenzi na mapambo pamoja na utengenezaji wa madirisha ya makaburi, likiwemo dirisha hili tukufu la bibi mtakasifu Zainabu mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Tunawashukuru sana ndugu zetu wanaofanya kazi katika Maqaam hii kwa juhudi nzuri za kudumisha mawasiliano, na kila aliyechangia mafanikio haya, kwa kujitolea mali au nguvu”.
Mwishoni mwa ujumbe wake Sayyid Adnani Mussawi akasoma mashairi aliyokua ameyaandika rasmi kwa ajili ya tukio hili, yasemayo:
Kwa utukufu wa Zainabu nakabidhi tuzo ya Abbasi *** Taji la undugu sio taji la Almasi.
Maana ya utumishi imeonekana yeye ni mtumishi wake *** Sio kila maana inaweza onekana kwenye karatasi.
Taji limepambwa tarehe kwa haiba yake *** Juu yake kuna aya zinazo angaza kama taa.
Baada yake ukafuata ujumbe wa Atabatu Zainabiyya tukufu ulio wasilishwa na Mheshimiwa Shekh Nabiil Halbawi, ameanza kwa kukaribisha wageni na kuishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu, akasema: “Shukrani zote ziwaendee Atabatu Abbasiyya na kiongozi wao mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, naye ni Muwakilishi bora wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Hussein Sistani, akawashukuru walio jitolea na walio tengeneza taji hili tukufu lililofunika kaburi la bibi Zainabu (a.s)”.
Akaongeza: “Shukrani za pekee ziwaendee waliokamilisha kazi hii tukufu, iliyofanywa kwa ustadi wa hali ya juu”.
Mwisho wa hafla mshairi Mula Ahmadi Bawi na Mula Khikani wakasoma tenzi kwa sauti nzuri zilizotaja utukufu wa bibi Zainabu (a.s).