Hatua iliyo fikiwa katika ujenzi wa sehemu kubwa ya dhahabu kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ameongea kuhusu kazi zinazofanywa katika mradi wa uwekaji mkubwa wa dhahabu katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamemaliza moja na hatua zake na kuelekea kwenye hatua nyingine ambayo ni paa la ndani, sehemu ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu.

Akasema kua: “Sehemu zilizo kamilika katika mradi huu ni:

  • - Kuzungushia ufito wa mapambo (uliotiwa dhahabu) unaozunguka mlango kwa nje, pamoja na mapambo mengine yaliyo buniwa katika awamu mpya ya utengenezaji wa mlango na yanayo endana na umbo lake.
  • - Kukamilisha uwekaji wa vipande vya dhahabu vilivyo nakshiwa sehemu yote hadi kwenye maandishi ya Quráni, nakshi hizo zinafanana na mapambo yaliyopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hivyo ndio vitu vilivyo ongezwa kwenye mradi huu.
  • - Kukamilisha kuweka maandishi ya Quráni yaliyo andikwa kwa hati ya Thuluthi iliyo shiba yasemayo (Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa, na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuwasaidia. * Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu..).
  • - Kukamilisha kuweka vifuniko vyenye nakshi ndani ya jengo katika sehemu ya mlango wa kuingia haram hadi kwenye maandishi ya Quráni, kukiwa na nakshi zingine zenye ufito wa maandishi yaliyotiwa mina ya bluu na kuna maandishi yaliyotiwa maji ya dhahabu yasemayo (Ewe mwezi wa bani Hashim).
  • - Kuweka maandishi ya Quráni pande tatu, maandishi ya upande wa kulia yanaukubwa wa (sm 351 x 70) imeandikwa surat Ikhlasi, upande wa ndani maandishi yanaukubwa wa (sm 700 x 70) imeandikwa sehemu ya aya ya (177) ya surat Baqara, na upande wa kushoto maandishi yanaukubwa wa (sm 349 x 70) imeandikwa surat Kauthara.
  • - Majina ya As-habul-Kisaa (a.s) kuanzia Mtume (s.a.w.w) hadi Imamu Hussein (a.s), yameandikwa ndani ya duara (lenye umbo la yai) la mzunguko wa bluu uliotiwa mina, na hati ya Thuluthu Jalliy iliyo shiba, katikati ya majina hayo kuna maneno yasemayo (Rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe kwenu watu wa nyumba ya Mtume hakika yeye ni mwingi wa kusifiwa na mwingi wa wema) katika umbo la peasi lenye kitako kilicho tiwa mina, maandishi hayo yamezungukwa na upinde mkubwa unao ungana na maandishi ya Quráni, na mwisho wake umekutana na mapambo mengine ya upinde.
  • - Kukamilisha uwekaji wa marumaru sehemu yote inayo tenganisha fito za mapambo na maandishi”.

Akasema: Hivyo ndio vipengele muhimu vilivyo kamilika, sasa hivi tumeanza kupamba paa la ndani, nayo ni hatua muhimu na ngumu katika mradi huu, inahitaji umakini mkubwa kutokana na wingi wa mapambo yake”.

Akamaliza kwa kusema: “Watekelezaji wa mradi huu ni Ataba tukufu chini ya utendaji wa raia wa Iraq wenye uzowefu mkubwa, baada ya kukamilika kwa mradi huu sehemu hiyo itakua na muonekano mpya, utakao ongeza uzuri wa eneo hili takatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: