Kiongozi mkuu wa kisheria ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona ambacho kimekamilika kwa asilimia 98

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi siku ya Alkhamisi ya mwezi (15 Shabani 1441h) sawa na tarehe (9 Aprili 2020m), amekwenda kuangalia hatua za mwisho za ujenzi, kwani umesha kamilika kwa asilimia 98.

Mheshimiwa amefuatana na katibu mkuu wa Ataba tukufu pamoja na makamo wake na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi pamoja na kiongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s).

Mheshimiwa amekagua hatua za umaliziaji wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ambacho kitakua sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa mtukufu wa Karbala, na akasikiliza maelezo kutoka kwa watekelezaji wa mradi.

Mjumbe wa kamati kuu ya uongezi Ustadh Jawadi Hasanawi amesema kua: “Tumefanya ziara hii kuangalia umaliziaji wa kazi za mradi huu muhimu kabla ya ufunguzi wake, ambao utakabidhiwa kwa mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala kama zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel, chini ya mkakari wa Atabatu Abbasiyya wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Kumbuka kua mafundi wanaofanya kazi katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, walianza ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona chini ya maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala na katika hospitali ya Hindiyya, kama sehemu ya kujiandaa kupokea wagonjwa wa virusi hivyo kama wakitokea (Allah atuepushie).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: