Mafundi wa idara ya viyoyozi (AC) chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wamefunga mtambo maalum wa kusafisha hewa katika kituo cha wagonjwa wa Korona, kinacho ungana na kituo cha Alhayaat katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala.
Idara hiyo imefunga mtambo wa kusafisha hewa kama ilivyo shauriwa na idara ya madaktari, kwani wagonjwa wanahitaji hewa safi.
Kupitia mtambo huo, vyumba vitakua na hewa safi kwa asilimia (%100) pamoja na maeneo mengine ya jengo, utasaidiana na mtambo wa kutoa hewa chafu amboa tayali umesha fungwa, hivyo kituo kitakua na hewa safi kwa asilimia (%100).
Muda wote mitambo hiyo itakua inasukuma hewa safi kutoka nje na kutoa hewa iliyopo ndani ambayo inaweza kua chafu, kazi hiyo itafanywa mara (20) ndani ya saa moja.
Kumbuka kua kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kimejengwa kama zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel kwa mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, na kitakua sehemu ya mji huo, watekelezaji wa mradi huo ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.