Mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel Dokta Jaasim Ibrahimi amesema kua idara ya afya ni mshirika mkubwa katika hospitali na lengo letu ni kuwahudumia watu wa Karbala.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kiitwacho (Jengo la Alhayaat la pili) katika mji wa Imamu Hussein (a.s), Ibrahimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hospitali wa rufaa Alkafeel inajivunia kutoa huduma bora, hakika idara ya afya ya mkoa wa Karbala ni mshirika wetu mkubwa, lengo letu ni kuhudumia mji wa Imamu Hussein (a.s) na kutoa huduma nzuri zaidi kwa wakazi wa mji huo”.
Akaongeza kua: “Hiki mnacho kiona hivi sasa, kukamilika ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ni uthibitisho wa ushirikiano uliopo kati ya hospitali ya rufaa Alkafeel na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, tunapenda uwe mfano wa ushirikiano mwema kati ya hospitali binafsi na idara ya afya”.
Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kiitwacho (Jengo la Alhayaat la pili), baada ya mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi kukamilisha ujenzi wa kituo hicho ndani ya muda wa siku kumi na tano, nayo hospitali ya rufaa Alkafeel imekitoa zawadi kwa mji wa Imamu Hussein hapa Karbala.