Kiongozi wa mji wa Imamu Hussein kitiba: Kituo kitaendelea kutoa huduma za afya hata baada ya kuisha tatizo la Korona

Maoni katika picha
Kiongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s) Dokta Swabahu Husseini amesema kua kituo kipya (Jengo la Alhayaat la pili) kilicho jengwa kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kitaendelea kutoa huduma ya afya hata baada ya kuisha ugonjwa wa Korona.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kiitwacho (Jengo la Alhayaat la pili) katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Kituo hiki kimejengwa kwa ajili ya kuhudumia watu wenye maradhi ya kuambukiza, ujenzi wake umezingatia utowaji wa huduma kwa watu wenye maradhi ya kuambukiza na kitaendelea kutoa huduma ya afya hata baada ya kuisha tatizo la Korona”.

Akaongeza kua: “Tunaishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na hospitali ya rufaa Alkafeel kwa kazi hii tukufu, bila kumsahau kila aliye changia ujenzi wa kituo hiki, ukizingatia kua kimejengwa ndani ya siku kumi na tato tu”.

Kumbuka kua kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kimetolewa kama zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel kwa mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, na jukumu la ujenzi likabebwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: