Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amesema kua kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona ni mafanikio makubwa katika kipindi hiki, ameyasema hayo katika ufunguzi wa kituo hicho (Jengo la Alhayaat la pili) katika mji wa Imamu Hussein (a.s) kilicho tolewa zawadi na hospitali ya rufaa Alkafeel.
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Kituo hiki ni hatua muhimu iliyofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kupambana na virusi vya Korona vinavyo endelea kusambaa katika mji wa Karbala, hususan inapo endelea kuongezeka idadi ya maambukizi, pia kituo hiki ni maendeleo makubwa katika kupambana na balaa hilo”.
Akaongeza: “Sio jambo geni kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya kila wawezalo katika kufanikisha mradi mkubwa kama huu ndani ya muda mfupi pamoja na ugumu wa mazingira ya kazi, ukizingatia kua kituo kipya kimejengwa upande kilipo kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, sambamba na uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi kutokana na marufuku ya kutembea iliyopo Karbala na sehemu zingine kwa ujumla”.
Akaendelea kusema: “Nawapa hongera watumishi wa afya wanaofanya kazi katika mji wa Imamu Hussein wa kitabibu, hatua hii na mafanikio haya ni kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa kazi zao katika kupambana na janga hili”.
Ujenzi wa kituo hiki ni sehemu ya kujiandaa kupokea idadi kubwa ya watu walio ambukizwa virusi vya Korona –Allah atuepushie-.