Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanaojenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali kuu ya Hindiyya kusini mwa mkoa wa Karbala, wamekamilisha ujenzi kwa zaidi ya asilimia (%75), ikiwa ni pamoja na ufungaji wa umeme.
Tumeongea na Mhandisi wa umeme Ustadh Hasanaini Haidari amesema kua: “Ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia (%75) ikiwa ni pamoja na kukamilika ufungaji wa umeme kwenye vyumba na sehemu zingine, tunamalizia kufunga nyaya sehemu chache zilizo bakia”.
Akaongeza kua: “Tumemaliza kuweka taa vyumbani na hivi sasa tumeanza kufunga feni za ukutani katika korido”.
Kumbuka kua mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, walianza kazi ya ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika eneo la hospitali ya Hindiyya mwezi (6 Shabani 1441h) sawa na tarehe (31 Aprili 2020m), kama sehemu ya kupambana na kuenea kwa virusi hivyo, kituo hicho kinajengwa katika eneo lenye ukubwa wa (2m1500) kina vyumba 35 pamoja na chumba cha usafi na dawa.