Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wamepiga hatua kubwa katika ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kinacho jengwa kwenye eneo la hospitali ya Hindiyya kusimi mwa mkoa wa Karbala, wamekamilisha ujenzi kwa asilimia (%80).
Mhandisi mkazi Ustadh Karari Barihi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Kazi inaendelea vizuri, tayali imesha kamilika kwa asilimia (%80), ukataji wa vyumba ukekamilika kwa asilimia (%100), ufungaji wa (Gypsam dord) umekamilika kwa asilimia (%100), huku ufungaji wa vifaa vya umeme ukikamilika kwa asilimia (%75), na leo tumeanza kufungo viyoyozi”.
Akaongeza kua: “Kazi za ujenzi wa chini zimekamilika kwa asilimia (%95) hali kadhalika utandikaji wa bomba za maji umekamilika kwa asilimia (%95) huku vyoo vikiwa vimekamilika kwa asilimia (%85), na kazi ya kupaka rangi imekamilika kwa asilimia (%85) na ujenzi wa dari umekalilika kwa asilimia (%35) hadi sasa”.
Kumbuka kua kituo kinajengwa sehemu ya wazi yenye ukubwa wa (2m1500) ambayo inaungana na eneo lingine kubwa la wazi lililo chini ya wanufaika wa mradi huu.