Mbele ya waziri wa afya wa Iraq: Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya ufunguzi wa jengo la Alhayaat la tatu katika hospitali kuu ya Hindiyya

Maoni katika picha
Alasiri ya Jumapili mwezi (2 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (26 Aprili 2020m) jengo la Alhayaat la tatu limefunguliwa rasmi, jengo hilo limejengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha usimamizi wa kihandisi, na limetolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel kama zawadi kwa hospitali ya Hindiyya, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mapambano dhidi ya virusi vya Korona.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na waziri wa afya wa Iraq na ugeni ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya ukiongozwa na katibu mkuu pamoja na makamo wake na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na baadhi ya marais wa vitengo vya Ataba, bila kusahau wawakilishi wa serikali ya mkoa wa Karbala na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama na kiongozi wa idara ya afya pamoja na mkuu wa wilaya ya Hindiyya.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu aliongozana na waziri pamoja na watu aliofuatana nao katika kukagua jengo hilo, akatoa maelezo kwa ufupi kuhusu wasifu wa jengo hilo, na namna watumishi wa Ataba walivyo kamilisha ujenzi ndani ya muda wa siku (24) tu, akabainisha kuwa hiki ni kituo cha tatu kujengwa ndani ya mwezi mmoja, baada ya kujenga kituo kama hiki kwenye mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, na kituo kingine katika mkoa wa Najafu, kilicho jengwa kwa ajili ya hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s), vituo vyote vimekabidhiwa idara za avya kwa ajili ya kuanza kuvitumia katika kutoa huduma, akamsisitizia kuwa Atabatu Abbasiyya inatekeleza maagizo yote ya kitabibu katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Baada ya kumaliza matembezi hayo wakafanya kikao na waandishi wa habari wa luninga, redio na magazeti, waziri alianza maelezo yake kwa kuisifu Atabatu Abbasiyya tukufu namna inavyo pambana na maambukizi ya virusi vya Korona, ambapo kielelezo halisi ni kituo hiki cha Alhayaat cha tatu, halafu akaeleza harakati za serikali katika vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona.

Mheshimiwa waziri wa afya Dokta Jafari Alawi amesisitiza kuwa: “Kukamilika kwa mradi mkubwa kama huu ndani ya muda mfupi ni jambo kubwa la kujivunia”.

Akongeza kuwa: “Bila shaka wataalamu hawa wanaweza kujenga vituo vya aina hii kwenye kila mkoa wa Iraq”.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar aliongea na vyombo vya habari, miongoni mwa aliyo sema ni: “Ujenzi wa vituo hivi umetokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, hatuwa ya kwanza tulianza kujenga kituo cha Alhayaat cha pili katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ambacho kilikamilika kwa muda mfupi sana, siku kumi na tano (15) tu, kikiwa na vyumba (57) vya wagongjwa ukiongeza na vyumba vya ofisi na dawa”.

Akasema: “Baada ya kumaliza ujenzi huo nguvu zikaelekezwa katika ujenzi wa Hindiyya kituo cha Alhayaat cha tatu, ambacho kimeongezwa kwenye hospitali ya wilaya hiyo ili kuongeza idadi ya vyumba vya kulaza wagonjwa (vitanda), kimejengwa kwenye kiwanja kinacho kadiriwa kuwa na ukubwa wa mita (1500) za mraba, jumla ya vyumba (35) vimejengwa”.

Akaongeza kuwa: “Vituo hivi viwili vimekabidhiwa idara ya afya ya mkoa wa Karbala kwa ajili ya kuvitumia kwa mahitaji yake, hususan katika mazingira haya, ujenzi huu umefuata tahadhari zote za kiafya”.

Kumbuka kuwa ujenzi wa vituo hivi ni sehemu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kupunguza msongamano kwenye kituo cha Alhayaat katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa wilaya ya Hindiyya ni miongoni mwa wilaya kubwa za mkoa wa Karbala na ipo kilometa (20) kutoka katikati ya mji wa Karbala, miradi imejengwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya na vimetolewa kama zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: