Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi amesema kuwa: Kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tatu kunaonyesha kuwa tunaweza kufanya kazi yeyote tutakayo pewa katika mazingira yeyote.

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Samiri Abbasi Ali amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tatu kumeonyesha wazi kuwa tunaweza kufanya mradi wowote wa ujenzi katika mazingira yeyote, mafundi wa kiiraq wanaweza kufanya kazi za kitaalamu.

Akaongeza kuwa: “Tumeweza kujenga kituo hiki ndani ya muda mfupi, tumejenga katika sehemu iliyokuwa na mahame yaliyo telekezwa kwa miongo mingi, ndani ya siku (24) tumefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kituo chenye vyumba (35) vya wagonjwa kwa ubora mkubwa”.

Akasema: “Kitengo hiki kimekidhi vigezo vyote vinavyo takiwa, kuanzia mfumo wa vyoo, viyoyozi, umeme pamoja na mifumo mingine yote”.

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya imefanya ufunguzi wa kituo hiki cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali kuu ya Hindiyya (kituo cha Alhayaat cha tatu) siku ya Jumapili mwezi (2 Ramadhani 1441h) sawa na tarehe (26 Aprili 2020m) mbele ya waziri wa afya wa Iraq, kimetolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel kama zawadi kwa hospitali kuu ya Hindiyya.

Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo hiki ni sehemu ya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Korona na kupunguza msongamano katika kituo cha Alhayaat kilichopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa wilaya ya Hindiyya ni miongoni mwa wilaya kubwa za mkoa wa Karbala, ipo umbali wa kilometa (20) kutoka katikati ya mji wa Karbala, kituo kimejengwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala chini ya usimamizi wa idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: