Leo siku ya Jumanne mwezi (2 Shawwal 1441h) sawa na (26 Mei 2020m) Atabatu Abbasiyya imezindua mradi wa nyumba za Alwafaa kwa ajili ya makazi ya familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji zilizo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Ataba tukufu.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Karbala na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na makamo wake, na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo, sambamba na viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.
Mradi huo upo katika mji mtukufu wa Karbala –mtaa wa Mulhaqu-, unalenga kutoa huduma kwa familia za mashahidi, umejengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (2500), pamejengwa nyumba nane zenye ukubwa wa mita za mraba (200) kila moja.
Tambua kuwa mradi huu ni sehemu ya ndogo ya kuonyesha thamani ya mashahidi watukufu walio jitolea kwa ajili ya taifa hili, na kusaidia familia ambazo zilikua tayali kupoteza wapenzi wao kwa ajili ya kulinda taifa, wananchi pamoja na maeneo matakatifu.