Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amesema kuwa, mradi wa Alwafaa wa nyumba za makazi ya familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, zilizo jengwa na kitengo cha uangalizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, ni sehemu ndogo ya kuonyesha kuzijali familia za mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda.
Akaongeza kuwa: “Hii ni hatua ya kwanza miongoni mwa hatua nyingi zijazo, mradi huu imeitwa (Nyumba za makazi Alwafaa wa kwanza), kuna miradi mingine itafuata kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.
Akabainisha kuwa: “Mradi huu unatoa ujumbe kuwa tunaweza kufanya kazi, kwa kushirikiana na kusaidiana na wadau wote wanao penda kuhudumia familia za mashahidi na majeruhi, kiwanja kilicho tumika kujenga nyumba hizo kimetolewa na mmoja wa waumini, na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wakajitolea kujenga, na pesa zilizo tumika zimetolewa na Marjaa Dini mkuu kupitia muwakilishi wake kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.
Akasisitiza kuwa: “Ujumbe mwingine ni kwamba mafundi na vijana wetu wanaweza kufanya miradi ya aina hii na kuimaliza kwa muda mfupi tena kwa ubora mkubwa”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumanne mwezi (2 Shawwal 1441h) sawa na tarehe (26 Mei 2020m) imefanya ufunguzi wa mradi Alwafaa ambao ni nyumba za makazi ya familia za mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji zilizo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Ataba tukufu.
Tambua kuwa mradi huu ni sehemu ni sehemu ndogo ya kuonyesha kujali kazi kubwa iliyo fanywa na mashahidi watukufu katika taifa hili, na kusaidia familia zilizo kubali kujitolea wapenzi wao kwa ajili ya kulinda taifa la Iraq, wananchi wake na maeneo matakatifu.