Atabatu Abbasiyya tukufu imefikia asilimia (%95) katika ujenzi wa kituo cha umeme

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa ujenzi wa kituo cha umeme umekamilika kwa asilimia %95, kituo hicho kitahudumia mkoa wa Karbala na kitasadia kuwa na umeme wa uhakika usio katika katika.

Akaongeza kuwa: “Mradi unajengwa katika (eneo la Zabaliyya) kwenye makutano ya barabara ya (Najafu – Karbala) na (Baabil – Karbala), ukubwa wa kiwanja ni mita za mraba (3000) eneo hilo linajengwa mambo yafuatayo:

  • - Jengo la kituo na limetumia sehemu kubwa ya kiwanja, jengo hilo limesanifiwa na kujengwa kwa namna inayo takiwa kwa ajili ya kituo cha umeme.
  • - Jengo la ofisi za kituo na limeungana na jengo la kituo, linavyumba vya ofisi mbalimbali.
  • - Nyumba nne za makazi ya watumishi wa kituo hicho.
  • - Sehemu ya bustani na matumizi mengine”.

Akasisitiza kuwa “Kituo hicho kimewekwa mitambo maalum, sehemu kubwa ya mitambo hiyo imetoka kwenye shirika la (Schneider Electric S.A) linalo husika na kutengeneza vifaa na mitambo ya umeme huko Ufaransa, miongoni mwa mitambo iliyo fungwa ni ile ya kufua umeme wa upepo, na mitambo yote inakidhi vigezo vya wizara ya umeme ya Iraq”.

Kumbuka kuwa kuanzishwa kwa kituo hiki ni mchango wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya umeme, kutokana na kukosekana kwa umeme wa uhakika na kuwepo kwa tatizo la kukatika katika kwa umeme, watekelezaji wa mradi huu ni shirika la Twayyiba baada ya kufanya makubaliano na idara ya umeme ya mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: