Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kinaendelea na ujenzi wa kituo cha kinywa na meno hapa Karbala

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya mambo ya nje chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea na kazi ya kujenga kituo cha kinywa na meno kitakacho kuwa chini ya kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi na ufundi, Mhandisi Samiri Abbasi amesema kuwa: “Siku ya kwanza ya mwezi wa sita mwaka wa 2020m, mafundi wa kitengo chetu walianza kazi ya ujenzi wa kituo hicho, jengo litakuwa la ghorofa nne (4), tabaka la chini litakuwa na mitambo ya upimaji (14), vyumba vya ofisi na sehemu ya vyoo, huku ghorofa la kwanza, la pili na la tatu kila moja litakuwa na mitambo (28) ya upimaji na sehemu mbili za vyoo”.

Akaongeza kuwa: “Tumeanza hatua ya kwanza ya kulisafisha, itafuata hatua ya kukata vyumba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa tofali”.

Akasisitiza kuwa: “Jengo litakuwa na vifaa vya kisasa vya umeme, viyoyozi, zimamoto, mfumo wa maji, pamoja na kutumia mfumo wa ulinzi wa kimataifa”.

Tambuka kuwa jengo hilo litasaidia kwa kiwango kikubwa kutoa huduma za ushauri na matibabu ya kinywa na meno kwa wananchi tena kwa kutumia vifaatiba vya kisasa zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: