Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) umesema kuwa wameanza kujenga sehemu ya kuoshea watu waliokufa kwa ugonjwa wa Korona kwenye makaburi maalum ya watu waliokufa kwa maradhi hayo katika mkoa wa Karbala, kwa kufuata kanuni za kihandisi na vigezo vilivyo tolewa na idara ya afya ya mkoa wa huo.
Tunafanya ujenzi huo baada ya kupokea maombi kutoka kwa wananchi, tunaiga uzowefu wa kikosi cha Imamu Ali (a.s) (Liwaau/2 Hashdu-Shaábi) katika makaburi ya Waadi-Salaam huko Najafu, pia tunaangalia uwezekano wa kufanya kazi zote, kuanzia kumuandaa maiti, kuchimba kaburi na kumzika.
Wajumbe wa kikosi cha Abbasi wamekutana na wawakilishi wa kituo cha afya walio ongozwa na Dokta Khalidi Aáraji ndani ya ofisi ya kikosi cha Abbasi na wamejadili utekelezaji wa mradi wa kuwasaidia wagonjwa wa Korona wanao ugulia majumbani mwao, kwa kuwafungia mashine za kusaidia kupumua na mahitaji mengine, kazi hiyo itafanywa chini ya uangalizi wa kitengo cha afya cha mkoa wa Karbala.
Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi Ustadh Maitham Zaidi amepongeza kazi nzuri inayo fanywa na majemedari wa jeshi leupe katika idara ya afya, na jinsi wanavyo thamini maisha ya wananchi kwa kufanya kazi saa 24 kila siku.