Atabatu Abbasiyya imeanza kufunga vifaa vya Oksijen katika mkoa wa Dhiqaar

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi asubuhi ya leo siku ya Jumatano mwezi (9 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (1 Julai 2020m) amesema kuwa mafundi wa kitengo cha uhandisi katika Atabatu Abbasiyya wameanza kufunga mitambo ya oksijen katika hospitali ya Hussein (a.s) mkoani Dhiqaar.

Akaongeza kuwa: “Kwa maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, mafundi wetu wameanza kufunga mitambo hiyo asubuhi ya leo siku ya Jumatano, baada ya kupata maombi kutoka kwa watumishi wa hospitali hiyo ya ulazima wa kupatikana mitanbo ya oksijen haraka iwezekanavyo, kutokana na kukosekana mitambo hiyo na umuhimu wa kutumika kwake katika kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona”.

Akasema: “Kila mtambo unauwezo wa kuzalisha mita (18) kwa saa, hivyo jumla ya lita (36) za oksijen zitazaliswa kwa saa”.

Akafafanua kuwa: “Tulitembelea sehemu hiyo siku tatu zilizo pita, tukaandaa vifaa hitajika kama vile viyoyozi na vifaa vingine kabla ya kuanza kazi ya kufunga mitambo hiyo, ambayo inatarajiwa kufunguliwa haraka iwezekanavyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: